UKWELI KUHUSU BIASHARA YA MTANDAO
Kutoka kwa dada @dianarosebardo
Mafanikio yako yanakutegemea wewe kwanza utakavyoweza kujitoa kujifunza na pia kufanyia kazi unavyofundishwa.
Sponsor, mdhamini yule mtu utakaeamua kumchagua ana mchango mkubwa sana katika wewe kufanikiwa. Huwa ni either ujijue una sponsor au huna kabisa.
Hapa upo online Unapenda ufanyaji biashara wa mtu, badala ya kumtafuta yule unaenda kwa mwingine wakati sababu kuu kwako kupenda biashara ilikuwa yule unaemuona kila siku, wewe hujiungi na company ni mtu.
Wengi huwa wanakosea hapa kwa kumuacha mhusika au sababu kuu yake na kwenda kutangatanga ila anapenda apate haki ya mafunzo, upendo na vile vinavyotokea kule kwenye sababu Halisia, akivikosa ataona anaonewa hafu biashara mbaya sana. Kumbe yeye ni sababu kuu.
Kukosea mtu wa kuwa mdhamini wako au sponsor au upliner au kiongozi hakujawahi kumwacha mtu salama katika hii biashara, labda kwa wale watu wachache ambao huwa exceptional ambao wanaamua to ku eat that ugliest frog
Kama bado hujaanza safari hii zingatia sana hili sio kila mzungu padri huhuhu. Nimemaliza
Comments
Post a Comment